kijana singida anyofolewa ulimi na mkewe
Kijana mkazi wa Unyakhae nje kidogo ya mji wa Singida, Said Mnyambi (26) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kunyofolewa kipande cha ulimi wake na mke wa jirani yake aliyekuwa anamlazimisha kufanya nae mapenzi.
Kwa mujibu ya maelezo ya kijana huyo, tukio hilo limetokea siku ya Idd El Haji Jumatatu wiki hii saa 3:30 usiiku.Alieleza kuwa siku ya tukio, mke wa jirani yao mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake, alimwomba amsindikize nyumbani kwa kuwa amelewa .
Alidai walipofika njiani,mama huyo alimtaka wafanye naye mapenzi jambo ambalo kijana huyo alimkatalia lakini alimwomba angalau waagane kwa kunyonyana ulimi (denda) naye akamkubalia.
Comments
Post a Comment